11/08/2026
Mwezi uliopita,Julai 2026 macho ya dunia yalikuwa nchini Uturuki, kwenye mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya mataifa ya magharibi (NATO). Miongoni mwao aliohudhuria mkutano huo ni Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye baada ya mkutano huo alitarajiwa kurejea nyumbani k**a kawaida. Lakini safari yake ya kurejea Marekani haikuwa ya kawaida kabisa.
Kwa mujibu wa taarifa ya The Washington Post, hofu ya uwezekano wa Iran kumlenga Trump wakati wa safari yake ya kurejea Marekani ilikuwa kubwa kiasi kwamba, licha ya kufika Uturuki kwa kutumia ndege mpya iliyotolewa na falme ya Qatar, Rais huyo hakurejea moja kwa moja Marekani akiwa ndani ya ndege hiyo.
Badala yake, maafisa wa usalama waliamua kutumia ndege ya zamani ya Air Force One, yenye rangi ya bluu na nyeupe, kusafirisha wafanyakazi wa Ikulu na waandishi wa habari. Hatua ambayo ilionekana kuwa sehemu ya mpango wa kiusalama ambao haukujulikana kwa watu wengi waliokuwa ndani ya ndege.
Video iliyorekodiwa siku hiyo inaonyesha Trump akipanda ngazi za Air Force One na kuwaaga watu waliokuwa uwanjani. Lakini muda mfupi baadaye, takribani dakika tano, waandishi wa habari walipanda ndege hiyo huku lori la huduma za chakula likiondoka eneo hilo.
Lori hilo lilionekana baadaye likielekea nyuma ya ndege nyingine ya kijeshi iliyokuwa imeegeshwa karibu na Air Force One. Na Taarifa zinaeleza kuwa Trump alikuwa ndani ya lori hilo la chakula na baadaye alihamishiwa kwenye ndege hiyo ndogo ya kijeshi, ambayo ilikuwa karibu na Air Force One.
Hatua hiyo ya kumhamisha Rais kwa siri inadaiwa kufanywa kwa lengo la kufanya safari yake isiwe rahisi , huku Air Force One ikiwa tayari inajulikana na kufuatiliwa kwa urahisi zaidi.
Taarifa hiyo inakuja wakati ambapo serikali ya Marekani imekuwa ikisisitiza kuwa kuna maadui wengi wa Marekani wanaomlenga Rais Trump, na kwamba vyombo vya usalama hutumia kila njia iliyopo kukabiliana na vitisho hivyo.
✈